Barua ya Mkurugenzi
Wakati wazo au ujumbe unawasilishwa, mwasilishaji lazima kwanza atathmini hadhira yake, kisha atengeneze ujumbe katika njia ambayo hadhira yake itaweza kuelewa. Hii inahitaji siyo tu kuwa na ujuzi mkubwa wa lugha, bali pia kuelewa vizuri kile ambacho msikilizaji anasikia/anafikiria wakati ujumbe unapopokelewa. Kazi yetu kama shule ya lugha ni kuwasaidia watu kupata ufahamu wa kutosha wa lugha ili waweze kuwasiliana kwa urahisi katika maisha yao ya kila siku. Hii inamaanisha ya kwamba tunalea wanafunzi wetu kwa makusudi maalumu katika kuwasaidia kuelewa lugha na utamaduni kwa kupitia vipindi vinavyohusisha wazawa wa lugha husika.
Sisi kama shule tunatambua uhitaji mkubwa wa watu kujifunza lugha ya Kiingereza kutokana na matumizi ya lugha hii katika maeneo mbalimbali. Ni muhimu kuwekeza muda katika kujifunza lugha tofauti na pia kuelewa utamaduni wa wazungumzaji wa lugha husika. Kwa bahati mbaya, watu wengi hutamani kujifunza lugha kwa haraka ili kuanza kuitumia moja kwa moja katika kazi zao mbalimbali. Lakini mara nyingi hawafanikiwi kufanya kazi zao hizo kwa ufanisi kutokana na uwezo mdogo wa lugha walionao. Ukosefu wa lugha ni suala lenye kukatisha tamaa hasa mtu anaposhindwa kuwasiliana vyema na wenzake. Sisi kama shule ya lugha tumetambua suluhisho la matatizo haya ya lugha na hivyo tunatumia mtaala mzuri wa kujifunzia lugha pamoja na walimu wenye ufanisi mkubwa katika kazi hii ili kuleta matokeo chanya. Ni vyema watu kufikiria kuwekeza vya kutosha muda wao katika kujifunza lugha tofauti. Tunaamini kwa kufanya hivyo tutaweza kwa pamoja kufikia maono yetu makubwa ya ustawi wa kujifunza lugha. Tafadhali turuhusu kukusaidia katika kuweka msingi imara wa kujifunza kwako lugha ya Kiingereza.